Kiswahili - Fasihi kidato cha Tano na sita

Kitabu hiki cha Kiswahili Kidato cha Tano na Sita Fasihi kina jumla ya sura tano. Sura hizo ni 

  1. Fasihi kwa ujumla, 
  2. Maendeleo ya fasihi simulizi
  3. Maendeleo ya fasihi andishi, 
  4. Uhakiki wa fasihi. na 
  5. Usanifu wa maandishi.

Kitabu hiki kimezingatia muhtasari wa somo la Kiswahili Kidato cha Tano na Sita wa mwaka 2009. Mada zote zimeandikwa kwa kina na zinanwhirikisha mwanafunzi kikamilifu. Maswali ya mazoezi na maswali ya marudio yameandaliwa kwa lengo la kumfikirisha na kumjengea mwanaftinzi umahiri katika somo. Hali kadhalika, lugha iliyotumika katika kitabu hiki ni rahisi na itakayomwezesha mwanafunzi kujifunza somo la Fasihi vizuri.

Kimeandaliwa na 

Taasisi ya Elimu Tanzania